KITENGO CHA ELIMU AFYA KWA JAMII - HOMA YA INI





 KITENGO CHA ELIMU AFYA KWA JAMII

SO.HI.CO.HE-rcce

UFAHAMU UGONJWA WA HOMA YA INI 


1.    UWAMBUKIZAJI

Ugonjwa wa Hepatitis b husababishwa na kirusi aitwaye hepatitis b virus (hbv). kirusi huyu huambukizwa kutoka mtu mmoja hadi mwingine kupitia:

·         Ngono Zembe: Unaweza kuambukizwa na mtu mwenye ugonjwa huo kama utajamiiana naye bila kutumia kinga na damu, mate, shahawa au maji maji ya ukeni yakaingia ndani ya mwili wako.

·         Kuchangia sindano: kirusi wa hepatitis b anaambukiza kirahisi sana kupitia sindano zenye damu ya mtu mwenye virusi hivi.

·         Mama kumwambukiza mtoto. mama mwenye mimba mwenye virusi vya hbv anaweza kumwambukiza kichanga wakati wa tendo la uzazi. mtoto anaweza kupewa chanjo baada ya kuzaliwa na akaepuka kuambukizwa, hivyo ni vizuri kuchukua tahadhari ya kujipima wakati una ujauzito

 

2.    DALILI ZA UGONJWA

Inaweza Kuchukua Siku 30 hadi 180 Kabla ya dalili Kutokea, watu Wengi hawana Dalili Mwanzoni Mwa Maambukizi. Wengine Huanza Kuugua Haraka Kwa: - 

  •  Kutoa mkojo mweusi na kupatwa na maumivu ya fumbatio.
  • Maumivu ya viungo (Joints)
  • Kukosa hamu ya kula
  • Kichefuchefu na kutapika
  • Udhaifu wa mwili na mwili kukosa nguvu
  • Macho na ngozi kugeuka rangi na kuwa vya njano

·        

3.    MADHARA YA UGONJWA

Kuwa na Hepatitis B kwa muda mrefu (Chronic Hepatits) kunaweza kusababisha madhara makubwa yafutayo ;

  • Kuvimba kwa ini kwa muda Mrefu Kunakotokana na Virusi wa Hepatitis B Kunaweza
  • Kusababaisha Makovu Kwenye Ini (Cirrhosis) na Kulifanya Ini Lishindwe Kufanya Kazi Yake inavyotakiwa. Liver Cirrhosis
  • Saratani ya Ini. watu wenye Hapatitis B Kwa Muda Mrefu Wanaweza Baadaye Wakapata Saratani Ya Ini.
  • Matatizo Mengine. Mgonjwa Mwenye Hepatitis B Anaweza Kupata Matatizo Ya Figo, Uvimbe Kwenye Mishipa ya Damu Na Upungufu Wa Damu.

4.    Tiba Ya Homa ya Ini

Magonjwa Mengi ya kinga huwaga hayana Tiba ivyobasi, Kwa mtu mwenye ilo gonjwa huwa wana onganishwa katika tiba  CTC.

5.    KINGA

Maambukizi Hayo yameweza kuzuiwa kwa Chanjo. Shirika la Afya Duniani (WHO) na wizara ya Afya kitengo cha Damu salama (MOH na NBTS) ambayo vinara katika makabailiano ya Ugonjwa wa Homa ya Ini aina ya Hepatitis B , wametoa mwongozo wake wenye mapendekezo ya Uchanjaji Watu wanaotakiwa Kuchanja: 

  • Mwananchi aliyezaliwa Chini ya Mwaka 2002
  • Mwananchi yoyote aliyepima nakupatikana Negative (-Ve) katika vipimo vya maabara na maabara inayoaminika

Mwaka 2013 Wizara ya Afya( MOH) pamoja na Mpango wa chanjo taifa (EPI) walizindua program mpya ya kukinga watoto , kwa kuchanja hep birth ( birth hepatitis ) hii ilipendekezwa kutokana na kuwa  ongezeko la watoto waliozaliwa kuzaliwa na hep positive, kupata kutoka kwa mama wakati wakujifungua.( * Research )

MAPENDEKEZO YA SHRIKA LA AFYA DUNIANI

WHO inapendekeza kwamba watoto wote wachanga wapokee chanjo ya hep birth (birth hepatitis) haraka iwezekanavyo baada ya kuzaliwa, ikiwezekana ndani ya saa 24, ikifuatiwa na dozi 2 au 3 za chanjo ya hepatitis B angalau wiki 4 tofauti ili kukamilisha mfululizo wa chanjo. Kinga hii hudumu miaka 20 , pia Shirika la Afya duniani haipendekezi chanjo za nyongeza kwa watu ambao wamekamilisha ratiba ya chanjo ya dozi 3.

Jedwali Na. Uchanjaji Pendekezwa Na Wizara ya Afya 



Reference / Vyanzo vya Taarifa:

(Hepatitis B - FAQs, Statistics, Data, & Guidelines | CDC, n.d.)

 

(Wizara ya Afya Tanzania 🇹🇿 [@wizara_afyatz], 2022)

(Hepatitis B, n.d.)

 

(Health | Ruvuma Region, n.d.)

 

(Health | Nyasa District Council, n.d.)


World Hepatitis Alliance



Comments

Popular Posts