"TUJENGE TABIA YA KUNAWA MIKONO, KWA WOTE "

Kuna sehemu nyingi ulimwenguni ambapo magonjwa yanayosababishwa na uchafuzi wa maji yameenea kama vile homa za matumbo, amabayo ni adui kwa watoto chini ya miaka 5 na  ujuzi ( afua) kuzuia haupatikani kwa wingi kwa jamii. Kwa zaidi ya SO.HI.CO.HE  ilitambua maeneo haya yenye changamoto na kushirikiana na wahudumu wa Afya ngazi ya jamii na kuhamasisha na kufundisha kanuni muhimu za usafi wa mazingira na Afya na kukusudia  kujenga teknolojia maalum ya maji katika maeneo ambayo upatikanaji wa maji ni magumu zaidi  ifikapo Agosti 2024 .

NYAKATI ZA KUNAWA MIKONO

  1. Baada yakupiga chafya /kukoa
  2. Baada ya kutoka chooni
  3. Kabla na baada ya kumsafisha mtoto aliyejisaidia 
  4. Kabla /wakati / baada ya kuanda chakula
  5. Kabla ya kula
  6. Kabla na baada ya Kumtembelea kumhudumia mgonjwa
  7. Baada ya kubeba na Kutupa taka
  8. Baada ya Kugusa vitasa vya mlango
  9. Baada ya kuwa kwenye maeneo ya umma 
  10. Baada ya kuwashughulikia wanyama

KANUNI ZA UNAWAJI WA MIKONO, KWA MAJI TIRIRIKA  NA SABUNI

1.Lowanisha mikono kwa maji safi tiririka 


2. Paka Sabuni kwenye sehemu zote za viganja na kutengeneza povu 


3.Sugua kiganja kwa kiganja huku ukipishanisha vidole


4.Sugua nyuma ya vidole kwa kutumia kiganja cha mikono mwingine


5.Sugua kila kifundo cha dole gumba 


6.Suuza mikono vizuri kwa maji tiririka, kisha kausha kwa tissue, ama kwa kutumia hewa/upepo

(Picha Chanzo: Simu ya Bw. Patrick.S )

KUWEKA ALAMA ZA KUHIMIZA TABIA YA KUNAWA MIKONO
(masinki ya kunawa  mikono) 
  • Shuleni /vyuo
  • Ofisini
  • Hopsital/ vituo vya Afya
  • Hotelini/ Nyumba za wageni
  • Gerezani/ vituo vya polisi
  • Stendi za mabasi 
  • Nyumba za ibada 






(an  ideal example, IEC of Bagamoyo Seafood and restaurant   ) 


ZINGATIA 

  • Kunawa Mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni kila unapotoka na kurudi nyumbani ili kjikinga wewe na familia yko dhidi ya magonjwa ya mlipuko 
  • Nyakati muhimu za kunawa mikono
  • Wajenge watoto tabia ya kunawa mikono mara kwa mara kwa maji titrirka na sabuni kwa kukuza ufahamu wa jinsi ya kunawa mikono kwa usahii ili kujikinga na magonjwa ya mlipuko 


Vyanzo:

(Nyumba Ni Choo – National Behavioural Change Campaign on Sanitation and Hygiene., n.d.)

(Kahn, 2019)

(Health Promotion, n.d.)

(Program: Elimu Ya Afya, n.d.)




Comments

Popular Posts